35 MBARONI WIZI WA VIFAA VYA SGR

 Shinyanga. Katika oparesheni ya mwezi Machi, Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata watuhumiwa 35 wa wizi wa vifaa vya SGR katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, pamoja kukamata jumla ya makosa 5,648 ya barabarani.

 

Akizungumza na vyombo vya habari leo Aprili 04, 2026 katika Ofisi ya polisi ya mkoa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema kuwa watuhumiwa wote wako katika mikono ya polisi kwa uchunguzi zaidi kubaini chanzo asili cha matukio hayo,

 

“Watuhumiwa 35 wanashikiriwa kwa wizi wa vifaa vya SGR ambavyo ni vipande vya nondo 306, bomba 32 za ukubwa wa mm12, stendi za makarasha 12 na bomba za mraba 65 katika eneo la Msalala na watuhumiwa wote wako mikononi mwa polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi” amesema Magomi.

 

Pia ameongeza kuwa, “Jumla ya makoza 5,648 yamekamatwa ambapo makosa ya magari ni 4,044 na makosa 1,604 ya bajaji na pikipiki ambapo wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa hapo” ameongeza Magomi.

Chapisha Maoni

0 Maoni