Iringa. Mfuko wa NSSF chini ya hifadhi scheme umefafikia kundi la watu waliojiajiri ili kuwekeza akiba kidogo kidogo ambapo mwanachama atanufaika na mfuko kwa kupata mafao ya uzeeni na mafao wakati wa matatizo kama magonjwa, shughuli za misiba na hata katika uzazi.
Akizungumza leo Machi 17, 2026 mkaguzi kutoka mfuko wa NSSF chini ya Hifadhi Scheme Elizabeth Mwankanye ameeleza kuwa mfuko huo kwa sasa umewafikia kundi maalum la waliojiari kama bodaboda, mamantilie, machinga na wafanyabiashara wote,
“Tulizoea kuona NSSF kwa walioajiriwa tu, sasa tumewafikia kundi maalum la watu waliojiri, hadi sasa tumesajiri vikundi 2,148 tumefanyikiwa kusajili kwa kuvitembelea vikundi hivyo na hadi sasa tuna jumla ya wanachama 5,632 na tunaendelea kutoa elimu kwa watu ili waweze kuweka akiba” amesema Mwankanye
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James ameeleza siri ya kupaa katika suala la maendeleo ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato bila ya kuwa kikwazo kwa wafanyabiashara ambapo imepelekea ukuaji wa viwanda na kuongezeka kwa pato la mkoa, pia ameeleza kuwa ongezeko la ukuaji wa idadi ya watu ni asilimia 2.4 kwa mwaka,
“Katika mkoa wa Iringa kuna kitu kimoja ambacho kimefanya kuwa na maendeleo makubwa ni pamoja na kulifanya lengo la ukusanyaji kodi kutokuwa kikwazo cha wafanya biashara, hii imepelekea walipo kodi kulipa kwa hiari” amesema James.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika nchini Tanzania (MISATan) Edwin Soko ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kukuza uhusiano mzuri kati ya waandishi wa habari na wadau wa habari hasa serikali ambao ni wadau wakubwa,
“Katika kongamano hili tunakuza mahusiano mazuri kati ya wadau wakubwa ambao ni serikali na waandishi wa habari pamoja na wahariri, ikiwa kazi kubwa ya vyombo vya habari ni kujenga na sio kubomoa” amesema Soko.
Pia kwa niaba ya wanachama ameongeza kuwa, “Nitoe shukrani kwa uongozi wa mkoa kwa kutoa nafasi ya kongamano hili kufanyika hapa na kutoa nafasi ya ujenzi wa ofisi yetu hapa kwa upande wa mikoa ya kusini mwa Tanzania” ameongeza Soko.




0 Maoni