RC JAMES AUNADI MKOA WA IRINGA, WINGI WA FURSA ZA KIUCHUMI

Iringa. Mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James ameeleza siri ya kupaa katika suala la maendeleo ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato bila ya kuwa kikwazo kwa wafanyabiashara ambapo imepelekea ukuaji wa viwanda na kuongezeka kwa pato la mkoa,


Akizungumza leo Machi 17, 2026 katika uzinduzi wa kongamano la wadau wa habari, wahariri na waandishi wa habari lililofanyika katika ukumbi wa mkoa wa Iringa uliopo Manispaa ya Iringa mkoani Iringa, pia ameeleza kuwa ongezeko la ukuaji wa idadi ya watu ni asilimia 2.4 kwa mwaka,


“Katika mkoa wa Iringa kuna kitu kimoja ambacho kimefanya kuwa na maendeleo makubwa ni pamoja na kulifanya lengo la ukusanyaji kodi kutokuwa kikwazo cha wafanya biashara, hii imepelekea walipo kodi kulipa kwa hiari” amesema James.


Pia ameongeza kuwa, "Pato la mkoa limeongezeka kutoka Sh. trilioni 4 hadi trilioni 6 kwa mwaka" ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika nchini Tanzania (MISATan) Edwin Soko ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kukuza uhusiano mzuri kati ya waandishi wa habari na wadau wa habari hasa serikali ambao ni wadau wakubwa,


“Katika kongamano hili tunakuza mahusiano mazuri kati ya wadau wakubwa ambao ni serikali na waandishi wa habari pamoja na wahariri, ikiwa kazi kubwa ya vyombo vya habari ni kujenga na sio kubomoa” amesema Soko.


Pia kwa niaba ya wanachama ameongeza kuwa, “Nitoe shukrani kwa uongozi wa mkoa kwa kutoa nafasi ya kongamano hili kufanyika hapa na kutoa nafasi ya ujenzi wa ofisi yetu hapa kwa upande wa mikoa ya kusini mwa Tanzania” ameongeza Soko.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Bodi ya maji bonde la Rufiji Jackline Baki ameeleza kuwa bonde hilo linahudumia zaidi ya mikoa kumi ikiwemo mkoa wa Iringa, pia kuna mradi wa mbinu asilia ya usimamizi wa vyanzo vya maji kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, ambapo kaya 12,000 zitanufaika na mradi,


“Mradi huo unatekelezwa katika eneo la Mbalali ambapo vinajengwa visima vya ulaguaji wa mito (Visima vya solar power) ambapo kaya 12,000 zitanufaika na mradi huo ambapo visima hivyo vitajengwa kwa wananchi kutumia badala ya kwenda katika chanzo cha maji cha bonde la mto Rufiji” amesema Jackline.


Chapisha Maoni

0 Maoni