WATUPWA JELA KWA KUTOA TAARIFA ZA UONGO

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.


Shinyanga. Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limetoa taarifa leo Aprili 09, 2026 ambapo wahukumiwa wawili ambao ni Kisaka Elinihaki (22) pamoja na Makoye James (20) wote wakazi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, watuhumiwa hao walidai kuwa sehemu zao za siri zimepotea kimiujiza baada ya kuguswa bega, jambo lililoleta taharuki kubwa katika jamii.


Baada ya kufikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama watuhumiwa hao walipatikana na taarifa za uongo zilizosababisha taharuki katika jamii, “Katika hukumu hiyo Kisaka Elinihaki alihukumiwa kifungo cha miezi sita huku Makoye James akihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela” Imesema taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imeongeza kuwa, “Jeshi la polisi linawakumbusha wananchi kutoa taarifa za uongo ni kosa la jinai na linaweza kusababisha taharuki katika jamii”


Aidha, limesisitiza umuhimu wa kutoa taarifa sahihi na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudumisha amani na utulivu.

Chapisha Maoni

0 Maoni