PROFESA MAHALU AMEFARIKI DUNIA

Profesa wa sheria na mwanadiplomsia Costa Mahalu (77) amefariki dunia

Taarifa kutoka kwa familia yake imethibithisha kwamba Profesa Mahalu amefariki dunia leo Jumatatu Machi 09, 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Alitambuliwa kama msomi mahiri, mwalimu mchapakazi na mwanadiplomasia mwenye uzoefu, aliyesaidia Tanzania kukuza elimu ya sheria na kuimarisha uwakilishi wake kimataifa.

Profesa Mahalu alizaliwa Julai 09, 1948 katika kijiji cha Katunguru wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza.

Chapisha Maoni

0 Maoni