Na Mwandishi Wetu.
Shinyanga. Aliyekuwa Mwenyekiti wa kuinusuru Timu ya mpira wa miguu Stand United (Chama la Wana) Issa Mbarak, ametangaza rasmi kuachana na shughuli zozote zitakazo husiana na timu ya Stand, kwa sababu ya kutokuwa na ushirikiano mzuri na manajimenti ya timu hiyo.
Akizungumza leo Mei mosi, 2026 na vyombo vya habari katika Manispaa ya Shinyanga Mbarak ameeleza kuwa, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti katika kikao maalum cha maridhiano ndani ya timu hiyo kilichoongozwa na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Salum Hamduni mnamo Novemba 14, 2025 na hivyo kufanyikiwa kuiongoza Stand kwa miezi minne tu,
“Nimekuja mbele yenu kutangaza rasmi kuachana na shughuli zozote zinazohusiana na timu ya Stand, ambayo niliteuliwa kama mwenyekiti kuiongoza Novemba, 2025 ambapo Februari, 2026 niliacha kujihusisha na timu hiyo na leo natangaza kuachana rasmi, kwa sababu za kutokuwa na ushirikiano mzuri na menejimenti ya Stand United” amesema Mbarak.
Pia ameongeza kuwa, “Wakati wa uteuzi wangu kama mwenyekiti wa kuinusuru Stand, niliteuliwa tu kwa maneno sikupewa uthibitisho wowote yaani barua, na ndio sababu ya mimi kutokuandika barua ya kujihudhuru” ameongeza Mbarak.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Said Mankiligo ameeleza kutokuwa na taarifa ya kutokuwa na maelewano mazuri kati ya aliyekuwa mwenyekiti Issa Mbarak pamoja na menejimenti ya timu ya Stand, pia ameeleza lazima aandike barua,
“Sina taarifa za Mwenyekiti wa kuinusuru Stand Mbarak kutokuwa na maelewano mazuri na menejimenti ya Stand, na pia kama anaachana na timu anatakiwa kuandika barua ya kujihudhuru na shughuli zozote zinazohusiana na Stand United” ameeleza Mankiligo.


0 Maoni