ASILIMIA 50 KUFIKIWA KAMPENI YA MSAADA WA HUDUMA YA KISHERIA (SAMIA LEGAL AID), SHINYANGA

 
Mkurugenzi msaidizi wa uzingatiwaji wa msaada wa huduma za kisheria kutoka wizara ya katiba na sheria Osborn Paissi.

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.

Shinyanga. Msaada wa kisheria kwa haki, usawa , amani na maendeleo kwa kuzingatia dira ya taifa ya mwaka 2050 kwa makundi ya watu muhimu kama wanawake, wazee, watoto na watu wenye ulemavu unatarajiwa kuzinduliwa rasmi kwa awamu ya pili Mei 6 hadi 20, 2026 kwa mkoa wa Shinyanga, ukiambatana na utoaji wa elimu kwa wananchi.

Akizungumza leo Mei 5, 2026 Mkurugenzi msaidizi wa uzingatiwaji wa msaada wa huduma za kisheria kutoka wizara ya katiba na sheria Osborn Paissi amesema kuwa katika kampeni hii ya awamu ya pili inatarajia kuwafikia asilimia 50 ya wananchi wa Shinyanga kwa kutoa huduma mbalimbali, 

“Tuna matarajio ya kuwafikia asilimia 50 ya wananchi wa Shinyanga kwa huduma za utoaji elimu ya kisheria, uandaaji wa masuala ya kisheria, kutoa uwakilishi wa mahakamani katika mabaraza, usajili wav yeti vya kuzaliwa na vifo sambamba na utoaji hati ya umiliki wa ardhi kwa muda mfupi” amesema Paissi.

Pia ameongeza kuwa, “Katika awamu ya kwanza yam waka 2023 asilimia 33 ya migogoro yote ilikuwa ni migogoro ya ardhi, ambapo katika kipindi hiki tumejipanga kutoa elimu ya umiliki wa ardhi na mipaka ya ardhi ambapo itasaidia kupunguza idadi ya migogoro ya ardhi” amesema Paissi. 

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema kuwa huduma hii itafanyika katika halmashauri zote sita za mkoa wa Shinyanga, hivyo wananchi wanatakiwa kufika katika vituo kupata utatuzi wa migogoro yao na kupewa elimu ya kisheria, 

“Manispaa ya Shinyanga kituo ni viwanja vya zimamoto katika eneo la Nguzonane, halmashauri ya Shinyanga vijijini vituo ni kata ya Didia uwanja wa shule ya msingi na Iselamagazi katika ofisi ya mtendaji wa kata" 

"Manispaa ya Kahama watakuwa kata ya Majengo national housing na kata ya Shunu eneo la ofisi ya mtendaji huku halmashauri ya Kishapu watakiwa Muhunze mnadani na kata ya Ukenyenge Community Centre, Msalala huduma itatolewa Segese uwanja wa shule na Isaka uwanja wa kosta pamoja na Ushetu katika kata ya Burungwa centre na Nyamilangano centre” amesema Mhita. 

MWISHO.

Chapisha Maoni

0 Maoni