21 MILIONI ZAREJESHWA TAKUKURU, SHINYANGA

Na Mwandishi Wetu,

Shinyanga. Katika kipindi cha mwezi Januari – Machi 2026 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga imeafnikiwa kurejesha kiasi cha Sh. 21,897,954/= milioni kutokana na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha, uchunguzi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii ikiwamo fedha kutokana na ushuru wa ujenzi wa shule kwa TRA.

Akizungumza leo Mei 29, 2026 na vyombo vya habari, Kamanda wa Takukuru mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy ameeleza kuwa hatua hiyo imekuwa ni mafanikio yaliyotokana na uelimishaji wa jamii kwa njia ya semina mbalimbali zilizotolewa ambayo imesaidia kuongezeka kwa uadilifu,

“Kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2026 Sh. 21,897,954/= milioni zimerejeshwa kupitia ufuatiliaji wa matumizi wa fedha, ambapo Sh. 5,540,254 milioni zimeokolewa kupitia ujenzi wa shule ya awali na msingi Tinde ‘B’, baada ya kubainika Sh. 5,316,304 ilipaswa kulipwa TRA ikiwa ni kodi na sh. 223,950 ushuru wa huduma kwa Halmashauri ya Shinyanga, sambamba na kiasi cha Sh. 9,672,000/= milioni zimeokolewa kupitia uelimishaji kwa njia ya semina kwa viongozi wa vyama vya msingi vya kilimo” amesema Kessy.

Pia ameongeza kuwa, “Tumefanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi 19 yenye thamani ya Sh. 3,906,564,882/= bilioni katika sekta ya elimu, afya, miundombinu na maji” ameongeza Kessy.

“Kupitia elimu kuhusu rushwa kwa AMCOS, imelipa madeni kiasi cha Sh. 9,322,000 milioni kwa makampuni ya Mwalata ililipa sh. 200,000 kwa Allience LTD, Ikoma ililipa sh. 1,150,000/= milioni kwa Mapacha, Wimate ililipa sh. 8,322,800 kwa kamouni ya 4CPRO Trade” ameongeza. 

Aidha wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga wameombwa kushirikiana kikamilifu na Takukuru katika juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa hududma za kijamii kwa ujenzi wa jamii yetu.

Chapisha Maoni

0 Maoni